Maandamano mengine huko Iraq ya Kusini:
11 Januari 2004Matangazo
BAGHDAD:
Mjini Amara huko Iraq ya Kusini, kwa mara nyingine wafanya maandamano miya kadha wamedai wapatiwe kazi na wanajeshi wa Kiingereza wanaoikalia nchi yao. Pia walilalamika kwamba wafanya maandamano hapo jana walitumiliwa mabavu na wanajeshi wa Kiingereza na polisi wa Kiiraq. Katika machafuko yaliyotokea hapo jana mjini Amarah kati ya wafanya maandamano na majeshi ya usalama, waliuawa watu watano na kujeruhiwa kadha wengine, waliarifu madakitari hospitalini. Baadhi ya watu walioshuhudia walisema polisi walikuwa wa kwanza kushambuliwa kwa risasi kutoka umati wa wafanya maandamano. Wengine wameripoti kwamba wafanya maandamano waliwashambulia kwa mawe polisi ambao walilipizia kwa kupiga risasi katika umati.