MigogoroMashariki ya Kati
Maandamano ya kutaka vita visitishwe Gaza yafanyika Israel
18 Agosti 2025Matangazo
Maandamano hayo yaliyoanza Jumapili asubuhi yanaupinga pia mpango wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu wa kuvitanua zaidi vita katika Ukanda wa Gaza.
Wakati huohuo wawakilishi wa kundi la Hamas wamelipokea pendekezo jipya la kusitisha vita kwa siku sitini Ukanda wa Gaza na kuachiliwa kwa mateka katika awamu mbili. Afisa kutoka kundi hilo aliyeomba kutokutajwa jina amesema pendekezo hilo linalosubiri kupitiwa na Hamas linatoa njia ya kuanzishwa kwa majadiliano yatakayovimaliza kabisa vita vya Gaza.