Maandamano makubwa huko Edinburgh , dhidi ya umasikini uliokithiri barani Afrika
3 Julai 2005Matangazo
Waandamanaji laki mbili wameteremka majiani katika mji mkuu wa Scottland Edinburgh,kuunga mkono mwito wa tamasha ya Live 8 kwa viongozi wa mataifa tajiri kwa viwanda kwaajili ya Afrika. Waandamanaji waliovaliaa nguo nyeupe walipaza sauti wakidai umaskini ukome.Maandamano na tamashasha za Live 8 zimeitishwa ili kuwazindua viongozi wa mataifa tajiri ya viwanda duniani G8 juu ya umaskini uliokithiri na hali mbaya ya maisha wanayokabiliana nayo wakaazi wa bara la Afrika.Viongozi wa G8 wanakutana wiki ijayo huko Ireland kuzungumzia misaada ya fedha kwa Afrika na namna ya kusamehewa madeni nchi masikini kabisa za dunia.