Maandamano makali dhidi ya Marekani yanaendelea Afghanistan
12 Mei 2005Maandamano yanayopamba moto dhidi ya Marekani nchini Afghanistan yamegharimu maisha ya zaidi ya watu watatu hii leo mashariki ya nchi hiyo.Wengi kadhaa wamejeruhiwa.Habari hizo zimetangazwa na maafisa wa serikali mjini Kaboul.Mamia kadhaa ya wanafunzi walikusanyika mbele ya chuo kikuu cha Kaboul na kuandamana hadi eneo la kati wakipaza sauti kuilaani Marekani.Wanalalamika dhidi ya ripoti ya kuchafuliwa kitabu kitukufu kwa waumini wa dini ya kiislam-Qoraan katika kambi ya kijeshi huko Guantanamo.Jana maandamano kama hayo mjini Jalalabad yalipelekea wanafunzi wanne kuuliwa na dazeni kadhaa kujeruhiwa.Wizara ya ulinzi ya marekani imethibitisha uchunguzi unafanywa kuhusiana na ripoti iliyochapishwa na jarida la Newsweek eti wanajeshi wa Marekani wamekua wakitupa misahafu chooni huko Guantanamo ili kuvunja hadhi ya imani yao ya kidini.