Kundi kubwa la upinzani Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo lafanya maandamano kupinga dhamira ya rais Joseph Kabila kutaka kusalia madarakani baada ya muda wake kumalizika mwishoni mwa mwaka huu.
Hata hivyo maandanamo hayo yamepigwa marufuku na serikali katika baadhi ya miji kama Goma na Lubumbashi lakini Kinshasa yameruhusiwa kufanyika. Kutoka huko Sudi Mnette amezungumza na mwandishi wetu Saleh Mwanamilongo.