Maandalizi ya kikao cha siri cha uchaguzi wa papa yaanza
5 Mei 2025Matangazo
Makadinali takriban 133 wenye umri wa chini ya miaka 80 wanatarajiwa kukusanyika katika kanisa la Sistine kuanzia siku ya Jumatano kumchagua kiongozi mpya wa kanisa Katoliki duniani, lenye waumini bilioni 1.4.
Soma pia:Makadinali wawili kukosa kongamano la kumchagua papa mpyaKikao cha siri cha kumchagua papa kinaweza kuendelea kwa duru kadhaa za upigaji kura hadi mgombea mmoja atakapofanikiwa kuungwa mkono na thuluthi mbili ya makadinali.
Wafanyakazi katika makao makuu ya kanisa hilo mjini Vatican tayari hii leo wamefunga pazia maalum kwenye roshani atakayosimama Papa atakayechaguliwa, katika kanisa kuu la mtakatifu Petro.