Maafisa wawili wakuu wa CHADEMA waliokamatwa wameachiliwa
25 Aprili 2025Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA kimesema viongozi wake wawili waliokamatwa na polisi wakiwa njiani kwenda mahakamani kuhudhuria kesi dhidi ya kiongozi wao wa chama ambaye anakabiliwa na mashtaka ya uhaini kwa kutaka mageuzi yafanyike kabla ya uchaguzi mkuu mwezi Oktoba wameachiliwa.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema liliwakamata viongozi watano wa chama hicho akiwemo Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania bara, John Heche na Katibu Mkuu wa chama hicho John Mnyika na baada ya mahojiano dhamana zao zikawa wazi.
Soma zaidi: Kesi ya Lissu chini ya ulinzi mkali jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu, alikamatwa Aprili 9 baada ya mkutano wa hadhara ambapo alitoa wito wa mageuzi ya uchaguzi.
Wanaharakati wa haki za binadamu wanaishutumu serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwabinya wapinzani, madai ambayo serikali ya nchi hiyo inayakanusha.