Maafisa White House wavujisha mipango ya kuishambulia Yemen
25 Machi 2025Maafisa wa juu wa utawala wa Trump wameripoti kuvujisha kimakosa taarifa za mipango ya siri ya kivita katika Group la mazungumzo la Signal, ambalo lilijumuisha mwandishi wa habari, kabla ya Marekani kuanzisha mashambulizi dhidi ya Wahuthi nchini Yemen.
Group hilo la mazungumzo, lililojumuisha maafisa wa juu kama Mshauri wa Usalama wa Taifa Mike Waltz na wengine, lilijadili maelezo ya kiutendaji kuhusu mashambulizi dhidi ya Wahouthi, na maoni yenye utata kutoka kwa Waziri wa Ulinzi Pete Hegseth kuhusu washirika wa Ulaya.
Soma pia: Jaji asema wahamiaji wanatendewa vibaya kuliko manazi na utawala wa Trump
Ingawa Hegseth amekanusha kuvujisha mipango ya vita, tukio hili limeibua wasiwasi kuhusu uvunjaji wa sheria za shirikisho zinazohusu taarifa za siri na uhifadhi wa rekodi. Hata hivyo Rais Trump amesema hana taarifa kuhusu uvujishaji huo, na kusema ana imani kubwa na timu yake ya usalama.