Marekani yashauri raia wake kuwa waangalifu nchini Uganda
6 Februari 2025Matangazo
Wamesema wanashirikiana na maafisa wa afya wa Uganda ili kukabiliana na tishio hilo.
Tahadhari hiyo ya usafiri, iliyotolewa na Kitengo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC), haijakataza safari za kwenda Uganda lakini inawashauri wasafiri kuchukua tahadhari, kama kuepuka watu wenye dalili za ugonjwa na kutotembelea vituo vya afya isipokuwa kwa dharura za matibabu.
Uganda yaanzisha chanjo ya majaribio ya kuzuia Ebola
Wiki iliyopita, maafisa wa afya wa Uganda waliripoti kuwa muuguzi mmoja katika hospitali moja jijini Kampala alifariki kutokana na Ebola. Hicho kilikuwa kifo cha kwanza kilichoripotiwa tangu mlipuko wa mwisho wa ugonjwa huo kumalizika mapema mwaka wa 2023.