Maafisa wa Lebanon na Marekani waijadili Kusini mwa Lebanon
5 Aprili 2025Matangazo
Taarifa kutoka ofisi ya rais imesema kuwa rais wa nchi hiyo, Joseph Aoun, na Ortagus walijadili kuhusu eneo la kusini mwa Lebanon, kazi ya kamati ya kimataifa ya ufuatiliaji mizozo na kujiondoa kwa Israel kutoka eneo la Lebanon.
Watu watatu wauwawa katika shambulizi la anga Lebanon
Katika taarifa, ofisi ya Waziri Mkuu Nawaf Salam, pia imesema mazungumzo na mjumbe huyo yalikuwa chanya.
Ziara ya pili ya Ortagus nchini Lebanon baada ya kuteuliwa kwake na Rais wa Marekani Donald Trump, inakuja katika wakati ambapo Israel inaendelea kufanya mashambulizi nchini Lebanon licha ya kusitishwa kwa mapigano na Hezbollah mnamo Novemba 27, na vikosi vyake vikisalia katika maeneo kadhaa kusini mwa nchi hiyo.