Vita vya Sudan ni "mzozo mbaya zaidi wa kibidamu duniani"
11 Februari 2025Mwenyekiti wa Jopo la Umoja wa Afrika kwa ajili ya Sudan Mohammed Ibn Chambas ameandika kupitia ukurasa wa mtandao wa X kuwa mapigano yanayoendelea yamefanya iwe vigumu kufikishwa msaada muhimu wa kiutu. Amesema hali hiyo imezidisha upungufu wa chakula na baa la njaa kwenye maeneo mengine ya Sudan na kwamba watoto na wanawake wananyanyaswa huru wazee na wagonjwa hawapati matibabu. Afisa mwingine wa umoja huo anayeshughulikia ustawi wa watoto Wilson Almeida Adao, amesema katika ujumbe tofauti kwamba idadi ya watoto wenye utapiamlo waliofikishwa hospitali nchini Sudan ilipanda kwa asilimia 44 mwaka 2024. Jeshi la Sudan limo vitani tangu Aprili 2023 dhidi ya wanamgambo wa RSF katika mzoto ambao umewalazimisha karibu watu milioni 12 kuyahama makaazi yao. Hivi sasa jeshi linadhibiti maeneo ya mashariki na kaskazini mwa nchi hiyo huku RSF wanadhibiti sehemu kubwa ya jimbo la Darfur.