Maafisa wa UN waonya juu ya mzozo nchini Kongo
20 Februari 2025Maafisa hao wametoa tahadhari hiyo kwenye mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumatano.
Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya kongo Bintu Keita amesema ni muhimu kwa baraza hilo kuchukua hatua za haraka na madhubuti ili kuepusha vita vya kikanda.
Mjumbe maalumu wa Ukanda wa Maziwa Makuu kwenye umoja huo Huang Xia kwa upande wake amesema hatua ya M23ya kuikanmata miji mikubwa mashariki mwa Kongo kunaashiria kitisho kinachoukabili ukanda huo kuliko awali.
Balozi wa Ufaransa kwenye umoja huo, Nicolas de Riviere amelitolea mwito baraza hilo kuidhinisha mara moja muswada wa azimio uliosambazwa na nchi yake wiki mbili zilizopita unaohimiza uungaji wake mkono wa uhuru wa Kongo, kumalizwa kwa mashambulizi ya M23, majeshi ya Rwanda kuondoka na kurejeshwa kwa mazungumzo.