MigogoroAfrika
M23 yakaribisha mpango wa mazungumzo na serikali ya Kongo
14 Machi 2025Matangazo
Katika taarifa, M23 imesema imepokea vyema tangazo hilo la mazungumzo yanayotarajiwa kufanyika mjini Luanda nchini Angola.
Hata hivyo, kundi hilo limeibua masuala kadhaa na kumtaka Rais wa Kongo, Felix Tshisekedi kueleza hadharani kujitolea kwake kwa mazungumzo ya moja kwa moja kama hatua ya lazima.
Awali Tshisekedi alikataa kujihusisha na mazungumzo ya moja kwa moja na M23, ambayo mara kwa mara ameitaja kama kundi la kigaidi.
Lakini siku ya Jumanne, Rais wa Angola Joao Lourenco, alisema mazungumzo ya moja kwa moja kati ya pande hizo mbili yatafanyika baada ya kufanya mazungumzo na Tshisekedi.