M23 wazidi kusonga mbele maeneo ya Kivu Kusini
18 Februari 2025Baada ya kuuteka mji wa Bukavu, waasi wa M23 waasi wanaonekana kuelekea njia tofauti. Kwanza kwenye barabara ya taifa namba tano inayoelekea wilaya za Uvira na Fizi hadi jimbo la Tanganyika. Mapigano makali yaliripotiwa siku ya Jumatatu katika kijiji cha Nyangezi kwenye barabara hiyo, kati ya M23 wanaoungwa mkono na Rwanda na jeshi la Kongo wakisaidiwa na jeshi la Burundi na wapiganaji wanaoitwa Wazalendo. Watu wawili wauawa Bukavu wakituhumiwa kuhusika katika uporaji
Walioshuhudia wanasema kuwa baada ya saa kadhaa jeshi la Kongo na askari wa Burundi walijiondoa kimkakati. Wakazi wengi walijifungia ndani ya nyumba zao, wengine wakihamia vijiji jirani. Nabintu ni mkazi wa Nyangezi ambaye amerejea kijijini kwake leo asubuhi baada ya kukimbia, anasema mapambano yamekwisha katika eneo lake.
Kwa mujibu wa mashuhuda mbalimbali, baada ya kukiteka kijiji cha Nyangezi M23 walielekea katika vijiji vingine vilivyoko kusini kuelekea bonde la mto Ruzizi. Jérémie ni mkazi eneo la Kamanyola lililoko kwenye mpaka kati ya Kongo, Rwanda na Burundi, anathibitisha kuwa hali hii imesababisha hofu miongoni mwa wakazi:Maelfu ya raia wa Kongo waomba hifadhi Burundi
Mashuhuda wanasema kundi lengine linaelekea kwenye barabara ya kitaifa nambari 2 katika wilaya ya Walungu, barabara hiyo inaelekea pia katika wilaya za Mwenga na Shabunda na inaendelea hadi jimbo la Maniema. Kundi lengine linasemekana kuelekea Bulambika kwenye barabara ya kitaifa nambari tatu inayounganisha miji ya Bukavu na Kisangani kupitia mbuga ya kitaifa ya wanyama ya Kahuzi-Biega.Vyanzo: Waasi wa M23 wameingia mji wa Bukavu
M23 wanaendelea Kivu Kusini huku katiba ya Kongo ikiadhimisha miaka kumi na tisa leo. Rais Félix Tshisekedi alikuwa ameelezea nia yake ya kuibadilisha kuanzia mwaka huu, akiamini kwamba iliundwa nje ya nchi na wageni na kwamba hailingani tena na ukweli wa sasa wa Kongo.
Baadhi ya Shughuli zafunguliwa
Shughuli za usafiri wa boti zimerejea leo kwenye Ziwa Kivu, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Bandari zimefunguliwa tena katika miji miwili ambayo imeangukia mikononi mwa waasi wa M23.
Umoja wa Mataifa umesema hatua hiyo itawezesha upatikanaji wa misaada ya kibinadamu baada ya wiki kadhaa za mapigano na uporaji.
Boti ya abiria kutoka Bukavu kwenda Goma iling'oa nanga leo asubuhi. Msimamizi wa boti hiyo Lweni Ndale, amesema hiyo ni safari ya kwanza kufanywa tangu mwishoni mwa Januari, muda mfupi baada ya mji wa Goma kuangukia mikononi mwa M23.Kongo yaukosoa Umoja wa Mataifa kwa kutochukua hatua kuhusu M23
Hata hivyo, uwanja wa ndege wa Goma, ambao Umoja wa Mataifa unasema ni muhimu sana kwa usambazaji wa misaada ya kiutu, bado umefungwa. Waasi wa M23 wakiungwa mkono na Rwanda wanajaribu kuonesha kuwa wanaweza kuiendesha miji ya Goma na Bukavu wakati maafisa wa Umoja wa Mataifa na serikali wakionya kuhusu janga linalokaribia la kibinaadamu, ikiwemo mlipuko wa kipindupindu na magonjwa mwengine.