MigogoroAfrika
M23 waishutumu Kongo kuhujumu mazungumzo ya Angola
17 Machi 2025Matangazo
Msemaji wa M23 Lawrence Kanyuka ameituhumu serikali ya Kongo kwa kutumia droni na ndege za kivita kushambulia kwa mabomu maeneo yaliyo na idadi kubwa ya watu katika siku za hivi karibuni.
Kanyuka amesema hatua hii ya serikali ya Kongo inaonyesha kwamba wana nia ya kuhujumu mazungumzo hayo yanayotarajiwa mjini Luanda.
Soma pia:Kagame aionya Ubelgiji kwa kuyachonganisha mataifa ya Afrika
Rais wa Angola Joao Lourenco alitoa wito wa usitishwaji mapigano kuanzia jana Jumapili ila pande zote hazikutoa tamko lolote kuhusiana na wito huo. Hata hivyo serikali ya Kongo ilithibitisha jana kuwa itawatuma wawakilishi wake katika mkutano huo.