Lula kukutana na rais wa Ureno
22 Aprili 2023Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva anatarajiwa kukutana na kiongozi wa Ureno leo hii katika safari yake ya kwanza barani Ulaya tangu aingie madarakani, ambayo inakuja huku kukiwa na mzozo na nchi za Magharibi kuhusu mtazamo wake wa hivi karibuni kuelekea vita vya Ukraine na Urusi.Mwanasiasa huyo wa siasa za mrego wa kushoto anaanza ziara ambayo ofisi yake imeiita mwanzo mpya wa mahusiano ya kidiplomasia wa Brazil, ikiwa ni baada ya miaka minne ya taifa hilo kutengwa chini ya utawala wa mtangulizi wake Jair Bolsonaro.Lula alirejea katika kiti cha urais mwezi Januari na kudhamiria kuirejesha Brazil katika jukwaa la kimataifa na hivyo kumchagua mtawala wa zamani wa kikoloni wa nchi hiyo Ureno kuwa kituo chake cha kuanzia Ulaya.Pia atazuru Uhispania katika ziara hiyo, ambayo inakuja baada ya safari za hivi karibu kwa mataifa ya China, Marekani, Argentina na Uruguay.