London.wanajeshi 14 wa jeshi la Uingereza wafariki katika ajali ya ndege.
3 Septemba 2006Matangazo
Wizara ya ulinzi ya Uingereza imesema kuwa wanajeshi 14 wa jeshi la nchi hiyo wameuwawa katika ajali ya ndege katika jimbo la kusini nchini Afghanistan la kandahar.
Msemaji wa NATO amesema ndege hiyo ilianguka kutokana na matatizo ya kiufundi, akisisitiza kuwa shambulio la wapiganaji sio sababu ya kuanguka kwa ndege hiyo.
Ajali hiyo inakuwa wakati mamia ya wanajeshi wa NATO na wa Afghanistan wameanzisha operesheni kubwa dhidi ya wapiganaji katika eneo linaloonekana kuwa ni ngome kuu ya Taliban.