LONDON:Uingereza yakana kuhusika na miripuko nchini Iran
17 Oktoba 2005Matangazo
Serikali ya Uingereza imekana kuhusika kwa njia yo yote ile na mashambulio mawili ya bomu yaliyofanywa kusini-magharibi mwa Iran na kuuwa si chini ya watu 4 na kuwajeruhi zaidi ya 100 wengine.Uingereza ilitamka hayo baada ya maafisa wa Iran kusema kuwa Uingereza iliwasaidia wanamgambo wa Kiarabu kufanya mashambulio hayo katika mji wa Ahvaz ulio na wakaazi wengi wa Kiarabu,karibu na mpaka wa Iraq.Maafisa hao wamesema,mabomu yalifichwa ndani ya mapipa mawili ya kutupia taka na yaliripuka wakati wa jioni ambapo watu wengi walikuwa njiani.Uhusiano kati ya Iran na Uingereza umezorota kwa sababu ya harakati za kinuklia za Iran na madai ya London kuwa Iran inawasaidia waasi nchini Iraq.