LONDON;Uingereza yaadhimisha mwaka mmoja tokea kushambuliwa na magaidi
7 Julai 2006Matangazo
Uingereza leo inaadhimisha mwaka mmoja tokea magaidi wafanye mashambulio kwenye kituo cha treni cha chini ya ardhi.
Watu 52 waliuawa katika mashambulio hayo na mamia wengine walijeruhiwa baada ya wanaitikadi kali wanne wa kiislamu kujiripua ,
Usalama umeimarishwa mjini London na idadi ya polisi imeongezwa ingawa idara ya usalama ya Scotland Yard imesema kuwa hakuna hatari yoyote.
Hatahivyo katika ukanda wa video uliotangazwa , kwenye televisheni ya Aljazeera , mmoja wa magaidi hao ,aliekufa, pamoja naibu kiongozi wa mtandao wa Alqaida bwana Ayman al Zawahiri wametishia kufanya mashambulio zaidi.