LONDON:Uingereza kuongeza majeshi nchini Afghanistan
11 Julai 2006Matangazo
Uingereza inapanga kupeleka wanajeshi mita tisa zaidi pamoja na helikopta kusini mwa Afghanistan.
Waziri wa Ulinzi wa Uingereza Browne amesema zoezi la kupeleka wanajeshsi hao litakuwa limekamilishwa hadi itakapofikia mwezi wa oktoba na hivyo kufanya idadi ya askari wote wa Uingereza nchini Afghanistan ifikie alfu nne na mia tano.
Askari wa Uingereza wanaongoza sehemu kubwa ya jeshi la NATO linalolinda amani kusini mwa Afghanistan.