LONDON:Mtuhumiwa wa mashambulio ya mabomu London adinda kurejeshwa Uingereza
31 Julai 2005Matangazo
Polisi ya Uingereza inawahoji watuhumiwa watatu wa mashambulio ya mabomu yaliyogonga mwamba mnamo july 21 mjini London,wakati ikiendelea kuwasaka waliopanga operesheni hiyo.
Mtuhumiwa wa nne wa mashambulio ya London amekiri kuhusika katika jaribio hilo lakini anapinga kurejeshwa Nchini Uingereza kutoka Italia alikokamatwa baada ya kufuatiliwa kupitia simu yake ya mkononi wakati akiitoroka Uingereza.
Hadi kufikia wakati huu watuhumiwa wote wanne wa mashambulio yaliyofeli ya juli 21 wametiwa mbaroni watatu mjini London na mmoja mjini Rome ltalia.