LONDON:Mtuhumiwa mwengine akamatwa nchini Uingereza
16 Agosti 2006Matangazo
Mtu mwengine amekamatwa na polisi nchini Uingereza kuhusiana na tuhuma za njama za kuripua ndege za abiria wakati zikiwa angani kuelekea Marekani.
Polisi imesema kuwa mtu huyo amekamatwa kutokana na kutuhumiwa kuchochea na kutayarisha kitendo cha ugaidi.
Watu wengine 24 wamewekwa ndani nchini Uingereza kutokana na tuhuma za mpango huo wa kushambulia ndege , uliogunduliwa mapema wiki jana. Idadi kubwa ya watuhumiwa hao ni waislamu.
Leo mawaziri wa mambo ya ndani wa nchi za Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kukutana mjini London ili kujadili masuala ya usalama kufuatia kugunduliwa njama hizo.