LONDON:Maandamano ya kupinga vita vya Iraq yafanyika
25 Septemba 2005Waziri mkuu Tony Blair anatazamiwa kuwa na wakati mgumu juu ya suala la vita vya Iraq baadae hii leo kwenye mkutano wa chama chake cha Labour.
Hii imekuja baada ya kufanyika maandamano makubwa ya kupinga vita vya Iraq mjini London ambapo waandamanaji wametaka kuondolewa mara moja kwa wanajeshi wa Uingereza nchini Iraq.
Maandamano hayo pia yamefanyika Marekani ambapo maelfu ya watu wameandamana mjini Washington kupinga vita hivyo vinavyoongozwa na Marekani.
Watu waliandamana nje ya ikulu ya Marekani wakimtaka rais Gorge Bush kuwaondosha wanajeshi wa Marekani huko Iraq.
Maandamano hayo yanafanyika hivi sasa huko San Francisco huku maandamano zaidi yakitarajiwa kwenye miji mingine ya Marekani.
Mikutano midogo ya kupinga vita hivyo imefanyika pia kwenye miji mikuu ya Denmark,Ufaransa na Korea Kusini.