LONDON:Kesho ni Uchaguzi mkuu Uingereza
4 Mei 2005Matangazo
Kampeini ya uchaguzi nchini Uingereza inamalizika leo huku uchaguzi mkuu ukitarajiwa kufanyika hapo kesho.
Katika kura ya maoni ya hivi karibuni inaonyesha kuwa waziri mkuu Tony Blair na chama chake cha Labour kinaongoza bila matatizo. Lakini hata hivyo mpinzani wake Michael Howard na Charles Kennedy wa chama cha Demokrats wanaendelea kufanya kampeini ya mwisho kwa bidii na juhudi zote.
Wanafanya kampeini hiyo katika maeneo amabako kura ya maoni inaonyesha kutiliwa shaka.Wapinzani wa Blair wamefanya kampeini zao kwa kuzingatia suala juu ya uamuzi wa Blair katika vita vya Iraq.hata hivyo Blair anatarajiwa kushinda katika uchaguzi huo kutokana na kunadi sera zake kwa kuzungumzia mipango ya kiuchumi.