LONDON:Bolton aishutumu Iran juu ya mpango wake wa Nuklia
15 Oktoba 2005Matangazo
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa John Bolton ameishutumu Iran kwa kujiingiza katika ushindani wa miaka 18 wa kutengeneza silaha za kinuklia.
Wakati huo huo Bolton amelezea matumaini yake kwamba hinikizo za kidiplomasia huenda zikaizuia Iran kufikia lengo lake la kutenegeneza silaha za Nuklia.
Bolton ametoa matamshi hayo alipokuwa ziarani Uingereza.
Awali mjini Paris Ufaransa ,waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condolezza Rice alisisitiza onyo la Marekani dhidi ya Iran kwamba ianzishe tena mazungumzo juu ya mpango wake wa Nuklia la sivyo ifikishwe mbele ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.