LONDON: Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza asema mashambulio ya London hayana uhusiano na vita vya Irak
18 Julai 2005Matangazo
Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza bwana Jack Straw ameyapuuza madai kwamba hatua ya Uingereza kuhusika katika vita vya Irak imeifanya nchi hiyo kuwa katika hatari ya kushambuliwa na magaidi.
Straw amelipinga dai lililotolewa na kampuni la Chatham House ambalo limeyahusisha mashambulio ya Julai saba mjini London na hatua ya Uingereza kuiunga mkono Marekani katika vita dhidi ya Irak mwaka wa 2003.