LONDON : Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Callaghan afariki dunia
27 Machi 2005Matangazo
Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza wa chama cha Labour James Callaghan amefariki katika mkesha wa kutimiza miaka 93 ya kuzaliwa kwake.
Callaghan amekuwa waziri mkuu hapo mwaka 1976 na kubakia madarakani kwa miaka mitatu ya vurugu kabla ya kushindwa katika uchaguzi na chama cha kihafidhina cha Margaret Thatcher.