LONDON Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza afariki dunia
18 Julai 2005Matangazo
Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Edward Heath amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 89. Akiwa mbunge wa chama cha kikosavativ kwa zaidi ya miaka 50, Heath aliingoza Uingereza kati ya mwaka 1970 na 1974.
Alijulikana sana kwa juhudi zake za kuongoza mazungumzo yaliyoiwezesha Uingereza kujiunga na jumuiya ya uchumi ya Ulaya mwaka wa 1973. Heath alishindwa kama kiongozi wa chama na Margaret Thatcher, aliyeitawala Uingereza kama waziri mkuu kwa awamu tatu.