LONDON: Watuhumiwa 9 watiwa mbaroni Uingereza
29 Julai 2005Matangazo
Polisi nchini Uingereza wamewakamata watu 9 wengine wanaotuhumiwa kuhusika na mashambulizi yalioshindwa kutekelezwa wiki iliyopita mjini London.Watuhumiwa hao wamekamatwa kusini mwa London.Maafisa wa polisi sasa,wamewazuia watu 20 kuhusika na mashambulizi ya London.Watu 3 kutoka jumla ya watuhumiwa 4 wakuu,wangali wakisakwa.Yasin Hassan Omar,ni mmoja aliekamatwa siku ya jumatano mjini Birmingham.Mkuu wa polisi wa London,Ian Blair ameonya kuwa makundi mengine huenda yakafanya mashambulio.